Mapato
Ingia

Bei

Bei moja, wazi, kwa maduka yako

Lipa kila mwezi, au lipa miezi 10 upate 12. Bei hazijumuishi VAT; VAT itaongezwa tu pale MOHD Technologies itakaposajiliwa kwa VAT.

Nyongeza ya miezi

Jaribu siku 10. Ukilipa mwezi wa kwanza, unapata miwili. Siku 10 zinabaki hata ukilipa siku ya kwanza.

Ukilipa kwa mara mojaMalipo ya kwanzaMalipo yanayofuata
Miezi 1 hadi 5+mwezi 1—
Miezi 6 hadi 9+miezi 2+mwezi 1
Miezi 10+miezi 3+miezi 2

Uaminifu: kila miezi 12 bila kukosa kulipia kwa wakati, mwezi 1 zaidi. Ukilipia zaidi ya siku 7 baada ya muda kuisha, hesabu inaanza upya (Waanzilishi: siku 40).

Maduka 10 au zaidi: ongeza TZS 50,000 kwa mwezi kwa kila kundi la maduka 10 (maduka 10 hadi 19 TZS 150,000; maduka 20 hadi 29 TZS 200,000).

Kukua hakufungi chochote. Ongeza duka na uendelee kufanya kazi: bei mpya inaanza baada ya siku za kusubiri malipo tu.

Tayari ni mteja? Unaendelea na bei yako ya sasa hadi tarehe 1 Juni 2027. Waanzilishi 100 wanaendelea na masharti yao.

Bidhaa za MOHD pamoja

Bidhaa mbili: unalipa jumla ya bei zake.

Chukua zote tatu, lipa mbili.

Ukiwa na Mapato, Maarifa na Maslahi, ya bei ndogo zaidi ni bure, kama nyongeza. Mfano: Maarifa Msingi TZS 50,000 + Mapato Msingi TZS 50,000 + Maslahi Msingi TZS 50,000 = TZS 100,000 kwa mwezi badala ya TZS 150,000. Inaendana na malipo ya mwaka pia. Inadumu wakati zote tatu zinalipiwa; moja ikisimama, inaisha siku ya kulipia upya inayofuata. Pesa hazirudishwi.

Una wafanyakazi 1 hadi 4? Maslahi (mishahara, kufuata sheria, wafanyakazi) ni bure kwako.

Mapato inajumuisha nini

Kila bidhaa ina kila inachohitaji kufanya kazi yake. Ukihitaji kazi kamili ya bidhaa nyingine, ni mpango wake, kwenye bili ileile.

Imejumuishwa: akaunti za wafanyakazi, majukumu, zamu; miongozo ya mafunzo ya wafanyakazi.

Mpango tofauti: mishahara na mawasilisho ya kisheria → Maslahi (bure kwa wafanyakazi 1–4).

Nyongeza za hiari (hizi tu)

SMS na WhatsApp za moja kwa moja (za kulipia kabla): TZS 20 kwa ujumbe.

Risiti za kodi za Mamlaka ya Mapato Tanzania: ada ya mshirika pamoja na faida ndogo.

Kifurushi cha kuanzisha (mara moja): takriban TZS 100,000 kwa mbali, pamoja na usafiri ukiwa eneo la kazi.

Hifadhi zaidi ya takriban GB 10: ada ndogo kwa kila GB 10.

Jina lako la tovuti kwa ukurasa wa umma: ada ndogo kwa mwaka (inakuja hivi karibuni).

Kila kitu kingine kimejumuishwa (kuhesabu stoo kwa AI, Uliza, ukurasa wa umma, usalama, nakala za akiba).

Waanzilishi 100 (biashara 100 za kwanza): bei yako haipandi maisha yote, maadamu unaendelea kulipa.

Malipo ya kwanza ya miezi 10 kabla ya 31/03/2027, ukitimiza vigezo vya bodi, nafasi zikiwepo.

Beji ya "Mwanzilishi #n".

Bei za mpango uliojiunga nao hazipandi maisha yote.

Kifurushi cha kuanzisha kwa mbali, bure.

Laini ya WhatsApp ya kipaumbele.

Vipengele vipya unavipata kwanza.

Mkutano wa waanzilishi kila robo mwaka.

Mwanzilishi mara moja, mwanzilishi kila mahali: masharti ya waanzilishi kwenye bidhaa nyingine yoyote ya MOHD utakayolipia kwa mwaka kabla ya tarehe ya kufunga.

Vipengele na bei yako vinafuata mpango unaoulipia.

Mpango wako unasimamiwa kwenye tovuti ya Mapato.

Mwenzako naye anapoteza mzigo bila kujua? Mpendekezee Mapato: duka hilo likianza kutumia Mapato, biashara yako na biashara hiyo kila moja inapata mwezi mmoja wa nyongeza. Shiriki kiungo kutoka Pendekeza Mapato ndani ya Mapato; kiungo hicho kinaonyesha kwamba duka hilo limetoka kwako.